Show simple item record

dc.contributor.authorObondo, Peres Akello
dc.date.accessioned2023-06-26T13:37:07Z
dc.date.available2023-06-26T13:37:07Z
dc.date.issued2023
dc.identifier.urihttp://ir.jooust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/12111
dc.description.abstractUtu huhusisha wema. Utu ni sifa mojawapo muhimu katika mahusiano mazuri maishani mwa binadamu. Utu ni sifa ambayo huhusishwa na wahusika mbalimbali katika dunia halisi na hata kwenye dunia ya fasihi. Wahusika ni muhimu katika fasihi kwa vile kupitia kwao, mwandishi huweza kupitisha ujumbe aliokusudia kwa wasomaji. Wahusika huwa wa aina mbalimbali wakiwemo wahusika wa kiuhalisiajabu ambao pia huchangia katika kupitisha ujumbe wa mwandishi sawia na wahusika wa kihalisia. Tafiti za awali zimewasawiri wahusika binadamu wakionyesha utu kwa sababu ni sifa muhimu anayopaswa kuwa nayo binadamu. Hata hivyo, waandishi wa Kiswahili akiwemo Said A. Mohamed wamesawiri wahusika wa kiuhalisiajabu wakionyesha utu kwa viumbe wengine. Huu ni mtindo ambao umeanza kutumiwa katika riwaya mpya na waandishi wa fasihi ya Kiswahili. Hivyo basi, utafiti huu ulichanganua kiuhakikifu wahusika viumbe wa kiuhalisiajabu katika riwaya teule za Said A. Mohamed ili kudhihirisha kwamba hata viumbe wasio binadamu huwa na sifa ya kibinadamu ya utu. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza utu wa wahusika viumbe wa kiuhalisiajabu katika riwaya teule za SaidA. Mohamed. Malengo yaliyoongoza utafiti huu ni: Kubainisha umbo linalochukuliwa na viumbe wa kiuhalisiajabu wanapoonyesha utu katika riwaya teule za Said A. Mohamed, kufafanua udhihirishaji wa utu wa viumbe wa kiuhalisiajabu katika riwaya teule za Said A. Mohamed na kutathmini athari ya utu wa viumbe wa kiuhalisiajabu kwa wahusika binadamu katika riwaya teule za Said A. Mohamed. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya kiuhalisiajabu kama inavyofafanuliwa na Zamora & Wendy (1995). Nadharia hii hueleza matukio katika hali ya kutisha, kushangaza na kuogofya kwa kuziwasilisha kana kwamba ni hali ya kawaida. Muundo wa kimaelezo ulitumika huku eneo la utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili, utanzu wa Riwaya. Mwango wa utafiti umehusisha riwaya zote tatu za kiuhalisiajabu za Said A. Mohamed. Sampuli ya kimakusudi ilitumika kuteua riwaya tatu za Said A. Mohamed hususan: Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Data ilikusanywa kutokana na kusoma riwaya hizo tatu zilizoteuliwa na kudondoa sehemu zilizolingana na malengo ya utafiti. Data ilidondolewa, ikanukuliwa, ikapangwa kasha kuchanganuliwa. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa kwa kweli viumbe wa kiuhalisiajabu wana sifa za utu kama upendo, ukarimu, kusamehe miongoni mwa mengine. Aidha walidhihirisha umbo mbalimbali kama kuwa kivuli,mizuka na mengineyo. Vile vile binadamu waliathirika kwa kufurahi na hata kukasirika. Utafiti huu unatoa mchango kwa walimu na wataalamu wa fasihi katika taaluma ya fasihi simulizi. Humanness involves any act related to wellness of a being. Being humane is an important aspect of life for healthy human relations. Humanness is related to various characters in the real world and in the literature world too. Characters are very important aspect of Literature. It is through characters that the writer conveys his intended message to the readers. There are many types of characters including magical realism characters through whom the writer, like the normal characters, conveys his message. Previous research have it that the humane character is only found in human beings. In as much as it is only found in human beings, some Kiswahili authors, among them Said A. Mohamed, have used non-human characters through magical realism to portray humanness. The art of writing using magical realism is a new style being used in literature by Kiswahili authors. This research therefore critically analyzes the humanness of nonhuman characters in magical realism to show that even non-human characters have humanness. The objectives of this study are to: identify and explain forms in which non-human characters in magical realism appear as they perform acts of humanity in Said A. Mohamed’s novels, describe ways in which they perform acts of humanness in Said A. Mohamed’s novels and the effect of humanness of these characters on human beings in Said A. Mohamed’s novels. This study uses Magical Realism theory as expounded by Zamora & Wendy (1995). This theory explains horrifying and fantastical scenes as if they are occurring in normal situations. This study employed descriptive research design while its area of study was the genre of novel in Kiswahili literature. The population of the study are all the 3 books of Said A. Mohamed that involve magical realism. Purposive sampling was used in selecting the three novels written by Said A. Mohamed; Babu Alipofufuka (2001), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010), because the writer has extensively expressed humanity through the non-human characters. Data was collected by reading the three selected texts. Excerpts were recorded, arranged as required and analyzed. The findings of the study show that non-human beingcharacters are humane as they show traits like love, generosity and even forgiveness. When showing these traits, they changed into different forms like shadows and even ghosts. The human beings reacted differently by being happy and some by being sad, after receiving these humane acts. This research will be beneficial to students, teachers and researchers of literature.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherJOOUSTen_US
dc.subjectUtuen_US
dc.subjectWahusikaen_US
dc.subjectKiuhalisiajabuen_US
dc.subjectSaid Ahmed Mohameden_US
dc.titleUtu wa Wahusika wa Kiuhalisiajabu Katika Riwaya Teule za Said Ahmed Mohameden_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record