Uchanganuzi wa Matini Zilizoteuliwa za Ugaidi Katika Gazeti la Taifa Leola Kenya Kati ya Oktoba 2010-Novemba2011.
View/ Open
Publication Date
2014Author
Type
ThesisMetadata
Show full item record
Abstract/ Overview
Vyombo vya habari nchini Kenya na kwingine ulimwenguni hutekeleza jukumu muhimu katika kuupasha umma habari za ugaidi. Uteuzi wa lugha katika kuripoti habari hizi ni muhimu katika kuwasilisha habari. Hata hivyo uteuzi wa lugha unaweza na athari mbalimbali kwa wasomaji wa habari za ugaidi. Hali hii inaweza kusababisha uadui, kutoaminiana na mielekeo hasi kuhusu baadhi ya watu katika jamii na hata dini. Utafiti huu umechanganua matini za ugaidi wa kitaifa na kimataifa katika gazeti la Taifa Leo linalochapishwa nchini Kenya. Lengo la utafiti lilikuwa kuchanganua usemi unaotumiwa kuripoti habari za ugaidi katika gazeti hili. Madhumuni mahsusi ni kuchunguza vipengele vya Jugha vilivyotumiwa kuwasilisha habari za ugaidi; kama uteuzi huo wa lugha ulikuwa na ishara za mwegemeo; kuhakiki athari ya habari hizo kwa wasomaji na kuchunguza namna sera ya uhariri ilivyoathiri uteuzi wa lugha. Nadharia Hakiki ya Uchanganuzi Usemi kama ilivyofafanuliwa na Teun van Dijk ( 1988), Norman Fairclough ( 1989) na Ruth Wodak (200 I) imetumiwa. Mu undo wa utafiti ni mseto wa Kipekuzi na Kimaelezo. Magazeti ya Taifa Leo yaliyochapishwa kati ya Oktoba 2010 hadi Novemba 2011 yamechunguzwa. Uchukuaji wa sampuli dhamirifu ulitumiwa ambapo magazeti yenye taarifa za ugaidi ndiyo yaliteuliwa na kuchunguzwa. Maoni ya wasomaji yarnekusanywa na kuchunguzwa kuhusu habari za ugaidi walizopokea. Jumla ya wasomaji 419 walishirikishwa katika uchunguzi. \Valiteuliwa kishalabela kutoka miji minne-Mombasa, Nairobi, Nakuru na Mumias ambayo ina wasomaji wengi zaidi wa gazeti hili. Miji hiyo inawakilisha maeneo ya Pwani, Kati, Bonde la Ufa na Magharibi nchini Kenya. Waandishi wa habari wanaoshughulikia habari za ugaidi nao walihojiwa. Waandishi hao wa habari waliteuliwa kimatilaba. Wale wote arnbao hushughulikia habari za ugaidi walishirikishwa. Data ya kithamano imechanganuliwa kwa uchunguza mawasiliano, maoni na majibu ya wasomaji. Data ya kiwingiidadi imewasilishwa katika majedwali na asilimia ili kuonyesha walioathirika na habari za ugaidi. Utafiti uligundua kwamba lugha inayotumiwa kuandika habari za ugaidi ina ishara za mwegerneo. Mwegemeo huo una athari hasi miongoni mwa wasomaji. Pia ilibainika kuwa mizozo hutokea kutokana na habari za ugaidi zilizosomwa kwenye gazeti hili. Vilevile kulikuwa na hali ya kushukiana miongoni mwa wasomaji kutokana na habari hizi, Sera ya karnpuni ya Nation Media nazo ziligunduliwa zinachangia katika uteuzi wa lugha mayoegemeza habari za ugaidi zinazochapishwa katika gazeti la Taifa Leo. Utafiti huu .imeangazia haja ya kufanya makini katika uteuzi wa lugha; vyanzo vya habari na nafasi ya uwasilishaji wa userni katika kuripoti habari za ugaidi iii kupunguza mwegemeo na athari hasi zinazosababishwa na mwegemeo huo. Unaweza pia kuchangia katika kuibua mtazarno ufaao kuhusiana na ugaidi na kwa hiyo kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi. Ufahamu wa utosha kuhusiana na swala la ugaidi ni hatua muhimu katika kupambana na ugaidi pamoja na athari zake.