Udhihirikaji wa Itikadi za Kisiasa Katika Midahalo ya Siasa za Uchaguzi wa 2022 Nchini Kenya Kupitia Jukwaa la Youtube
Publication Date
2025-01Author
Type
ArticleMetadata
Show full item recordCitation
Aboge, N. A., Miruka, F. & Akinyi, J. J.(2025). Udhihirikaji wa Itikadi za Kisiasa Katika Midahalo ya Siasa za Uchaguzi wa 2022 Nchini Kenya Kupitia Jukwaa la Youtube.East African Journal of Swahili Studies, 8(1), 17-31. https://doi.org/10.37284/jammk.8.1.2576
Abstract/ Overview
Makala hii inalenga kudhihirisha kuwa itikadi ni dhana ya kimsingi na haina budi kuibuka kila wakati mwanasiasa anapozungumza wakati wa kampeni akiwa na nia ya kujielekezea mamlaka. Itikadi inayoibuka kutoka kwenye hotuba, midahalo na mitafaruko ya kiuneni kati ya wanasiasa nyakati za kampeni za kisiasa ndizo huelekeza mienendo, maoni, mitazamo, Imani, fikra na mifumo ya mawazo ya wananchi wapigaji kura kiasi cha kuathiri uamuzi wao wa kiongozi wanaomtaka katika uchaguzi. Ni katika hali hii ndipo mwanasiasa fulani hupendelewa zaidi ya mwengine, ikizingatiwa kuwa itikadi ya mmoja imeridhisha ikilinganishwa na ya mwengine.Katika mkabala huo, makala hii ina nia ya kudhihirisha itikadi mbalimbali za kisiasa zilizoibuka kutokana na midahalo ya siasa za 2022 nchini Kenya kama zilivyojitokeza katika jukwaa la youtube. Kupitia midahalo tajwa, makala hii inatarajia kuthibitisha kuwa itikadi ndiyo dira inayoelekeza kupendwa au kuchukizwa kwa sera za wanasiasa, na hivyo kuathiri uchaguzi na matokeo yake.