Show simple item record

dc.contributor.authorMiruka, Frida Akinyi
dc.date.accessioned2022-11-17T17:11:48Z
dc.date.available2022-11-17T17:11:48Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://ir.jooust.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/11589
dc.description.abstractMafumbo yameainishwa kama kipera cha semi za fasihi simulizi za Kiswahili. Licha ya hali hii ni utanzu changamano wenye vipashio vya lugha na tanzu nyingine za fasihi. Hivyo yanatumiwa kwa upana katika matini semwa na andikwa na hivyo kujitokeza katika maneno, vishazi, tamathali za usemi na maumbo ya tanzu nyingine za fasihi. Kyallo Waddi Wamitila ni mmoja wa wataalamu wa fasihi ya Kiswahili waliofafanua na kuainisha mafumbo kama semi. Kadhalika ameandika kazi za sanaa zikiwerno tamthilia arnbamo anatumia mafumbo kwa upana unaozidi semi. Ni katika msingi huu ambapo utafiti huu uliazimia kuchunguza mafumbo katika tamthilia za Wamitila iii kuyaainisha. Matini zilizochunguzwa ni Wingu la kupita (1999); Pango (2003); Sumu ya Bafe (2006) na Seserumbe (2006). Madhumuni mahsusi yalikuwa kuchunguza rnabadiliko katika dhana na umbo la mafurnbo katika tamthilia za Wamitila, kutathmini matumizi ya mafumbo kama mtindo katika tamthilia za Wamitila na kupendekeza vigezo vya uainishaji wa rnafumbo katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Dhana ya Mafumbo ya Lakoff na Johnson (1987). Mihimili ya nadharia iliyotumika ni kipengele cha mabadiliko katika dhana ya fumbo, hoja ya maenezi, hoja ya mak:undi na hoja ya ulinganifu. Muundo wa kiuchanganuzi uliturnika huku eneo Ia utafiti likiwa fasihi ya Kiswahili utanzu wa tamthilia. Utafiti ulilenga matumizi ya lugha kisanaa katika tamthilia za Wamitila. Sarnpuli dabwa dabwa ilitumika kuteua tamthilia za Wamitila huku sampuli rejelevu na mjazo ikitumika kuteua mafumbo iii kuchanganuliwa. Data ilikusanywa kwa udurusu na uchanganuzi wa matini nayo mbinu ya unukuzi ikitumiwa k:udondoa sehemu za matini na kuwekwa kwenye jedwali la matukio. Uchanganuzi kithamano ulifanywa kwa mtinclo wa uchanganuzi wa yaliyomo huku kipengele cha uchanganuzi kikiwa matini zenye kufumba maana. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa mafumbo yamebadilika kwa kuchukua maumbo ya tanzu nyingine kama hadithi, mashairi, nyimbo na mazungumzo, Pili, ilibainika kuwa mafumbo yametumika kama mtindo katika tamthilia za Wamitila kwani tarnthilia zote zilionyesha mtindo wa mafumbo ya kihadithi, kishairi, nyimbo, mazungumzo na tamathali za usemi kama tashbihi na uhuishi, Kutokana na mabadiliko katika umbo na matumizi ya mafurnbo katika tamthilia za Wamitila, utafiti ulipendekeza vigezo vitatu vya uainishaji wa mafumbo. Kwa msingi wa kigezo cha tanzu, mafumbo yaainishwe kama mafurnbo ya kitamthilia, mafumbo ya kihadithi, mafumbo ya kishairi mafumbo ya nyimbo na mafumbo ya kimazungumzo. Kigezo cha kitarnathali kiainishe mafumbo ya kimethali, mafumbo ya kitashbihi, mafumbo ya kisitiari na mafumbo ya nahau. Hatimaye kigezo cha kiistilahi kiainishe mafumbo ya kiistilahi. Hivyo basi utafiti ulihitimisha kuw= rnafumbo yamebadilika kimaumbo na kimaturnizi hivyo kupita mpaka wa semi za fasihi simulizi. Utafiti unapendekeza kuwa uainishaji wa mafumbo katika fasihi ya Kiswahili uzingatie vigezo vilivyopendekezwa na dhana ya mafumbo ipanuliwe kuhusisha 'matini zozote zenye kuzua ulinganishi kwa njia fiche'. Utafiti huu huenda utawafaa wasorni, wahakiki na wanafunzi wa fasihi katika viwango vyote vya elimu. Utawawezesha kuelewa zaidi dhana na vigezo vya uainishaji wa mafumbo.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherJOOUSTen_US
dc.titleVigezo Vya Uanishiji wa Mafumbo Katika Fasihi ya Kiswahili: Uhakiki wa Tamthilia za Kyalo Waddi Wamitilaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record