Usawiri wa Vijana wa Kisasa katika Riwaya ya Dunia yao ya Kiswahili.

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Nature and Science Organization.

Abstract

Makala hii itachunguza usawiri wa vijana katika dunia ya sasa inayobadilika kila uchao. Itafanya hivi kupitia uchanganuzi wa riwaya mpya ya Dunia Yao (2006) ya S.A Mohamed. Utafiti unaonyesha kwamba vijana kote duniani sasa wana utamaduni wao ambao watafiti wanaueleza kama ‘ulimwengu huru’ wa vijana ulio na mitindo na njia za maisha ambazo, vijana hufuataili kujitofautisha na utamaduni wa wazazi wao. Utamaduni wa vijana kwa kiasi kikubwa ni zao la maendeleo katika jamii za ulimwengu. Kadri jamii inavyosonga mbele kimaendeleo, ndivyo ambavyo utamaduni wa vijana unakuzwa, unaimarishwa na kusambazwa miongonimwa vijana kote duniani. Vijana wamebuni utamaduni wao kama njia moja ya kuasi dhidi ya utamaduni uliotawaliwa na wazee. Wanataka kujihusisha na tabia kama matumizi ya dawa za kulevya, ushoga, uasi wa maadili ya kijamii, Mitindo mipya ya mavazi, muziki miongoni mwa tabia nyingine ambazo wanajua huwatenga wazee. Hii ni tabia ibuka ya vijana kupania kuonyesha nguvu na uwezo wao katika jamii. Ujumbe wanaopitisha ni kuwa hawako tayari kushiriki utamaduni unaowadhibiti na kuwanyima nafasi yao katika jamii. Malengo mahususi yatakayoongoza makala haya ni pamoja na kuangazia sifa za vijana wa kisasa na wakati huo huo kufafanua njia mabazo wanajamii wanaweza kutumia ili kujaribu kuziba mwanya mpana uliopo kati ya kizazi cha jana na cha leo. Makala hii itaongozwa na nadharia ya uhalisia. Mhimili mkuu wa nadharia ya uhalisia ambao utaongoza makala ni kwamba, fasihi ni kioo cha jamii na inapaswa kumulika maisha kama yalivyo. Muundo wa kimaelezo utatumika kuchanganua data. Data itakusanywa kutokana na kusoma riwaya teulena kudondoa sehemu zinazolingana na malengo ya utafiti. Data itadondolewa, itanukuliwa, itapangwa kisha kuchanganuliwa kulingana na mada husika.

Description

Keywords

Usawiri wa Vijana, Usawiri wa Vijana, Riwaya ya Dunia yao, Kiswahili

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By